IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon

Mgogoro baina ya Mashia na Masuni ni kwa maslahi ya Israel

12:58 - June 06, 2015
Habari ID: 3311306
Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Gebran Bassil amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unafaidika sana na mgogoro baina wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni.

Basil amesisitiza umuhimu wa umoja miongoni mwa Waislamu na kuongeza kuwa nchi za eneo zinapaswa kuwa macho kuhusu maadui wanaoenzea chuki na migongano baina ya Waislamu.
Amenukuliwa na tovuti ya al-Nushra akisema, Waislamu wawe ni Mashia au Masuni wana azma kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na kwamba hakuna tafauti baina yao kuhusu vita dhidi ya magaidi.
Bassil ameashiria hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Lebanon katika vita dhidi ya magaidi wa Kitakfiri na kuongeza kuwa, kila moja katika jeshi hilo linalojumuisha Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni na pia wafuasi wa dini za Kikristo na Kidruze wote wako mstari wa mbele kupambana na ugaidi.
Magaidi wa Kitakfiri na Kiwahabi wa kundi la Daesh  au ISIL wamekuwa wakiendesha uhalifu na ugaidi katika mpaka wa Lebanon na Syria na katika siku za hivi karibuni Jeshi la Lebanon limefanikiwa kuwapa pigo kubwa magaidi hao wa kitakfiri.../mh

3311158

captcha