IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani huko Najaf, Iraq

15:52 - September 11, 2024
Habari ID: 3479416
IQNA – Toleo la tano la Mashindano ya Qur’ani yaliyofanyika katika mji mtakatifu wa Najaf, Iraq, lilifikia tamati katika sherehe zilizofanyika wikendi.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Majlisi ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu yenye mfungamano na Mfawidhi wa Haram au kaburi takatifu la Hadhrat Abbas (AS) chini ya usimamizi wa Taasisi ya Kufundisha Qur'ani ya Najaf Ashraf.

Jumla ya wahifadhi 113 wa Qur'ani kutoka taasisi na vituo tofauti vya Qur'ani vya Najaf walishiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani, wakishindana katika duru za awali na za mwisho.

Kategoria hizo zilikuwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima na kuhifadhi, Juzuu 20, 10 na tano za Qur'ani Tukufu.

Sherehe zilianza kwa usomaji wa aya za Kitabu Kitakatifu na qari na mhifadhi wa Qur'ani Muhammad Ridha Ibrahim.

Kisha, Muhnad al-Mayali, mkurugenzi wa Taasisi ya Qur'ani ya Najaf Ashraf, alitoa hotuba ambayo alisifu kiwango cha juu cha washindani na shauku yao ya kujifunza Qur'ani.

Vile vile amesisitiza umuhimu wa tukio hilo la Qur'ani kwa ajili ya kuendeleza ujuzi na uwezo wa wanaharakati wa Qur'ani na kuwatayarisha kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa.

Mwishoni mwa sherehe, washindi wa daraja la kwanza hadi la tatu walitajwa na kupokea zawadi na vyeti vya heshima.

4235829

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu najaf
captcha