Taasisi ya Qur'ani Tukufu, yenye uhusiano na idara hiyo, huandaa vikao kila wiki.
Vikao hivyo vinalenga kukuza ujuzi wa Qur’ani miongoni mwa maqari wa jiji hilo, kulingana na tovuti ya idara hiyo.
Katika kila kikao, maqari husoma aya za Qur’ani Tukufu na kisha Sheikh Mahdi Qalandar, mkufunzi mtaalam wa Qur'ani, hutoa tathmini yake ya utendaji kwa mujibu wa kanuni za Qiraa, Waqfu, Ibtida, Sawt na Lahn, Ali al-Zubaidi, afisa wa taasisi hiyo alisema.
Ameongeza kuwa, sehemu ya kikao hicho pia ina visomo vya Qur'ani vya maqari mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu.
Amebainisha kuwa tawi la taasisi hiyo mjini Najaf huandaa vikao vya kila wiki vya Qur'ani.
Shughuli za Qur'ani zimeendelea kwa kiasi kikubwa nchini Iraq tangu kupinduliwa kwa dikteta wa zamani Saddam Hussein mwaka 2003.
Kumekuwa na mwelekeo unaokua wa programu za Qur'ani kama vile mashindano, vipindi vya kisomo na programu za elimu zilizofanyika katika nchi hiyo ya Kiarabu katika miaka ya hivi karibuni.
3490515