Baraza la Sayansi ya Qur'ani, lenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hazrat Abbas (AS) limeanzisha vituo vya Qur'ani katika siku ya 28 ya mwezi wa Hijri wa Safar, kwa mujibu wa tovuti ya al-Kafeel.
Siku hiyo ambayo imeadhimishwa leo Jumatatu, Septemba 2, ni kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wake, Imam Hassan (AS).
Sayyid Ahmed al-Zamili, afisa wa taasisi ya Qur'ani ya Astan amesema zaidi ya wataalamu 30 wa Qur'ani wapo katika vituo vya Qur'ani kwa ajili ya kuwasaidia wafanyaziara katika Haram Tukufu ya Imam Ali (AS) kusahihisha makosa yao katika usomaji wa Sura za Qur'ani Tukufu.
Pia wanajibu maswali ya waumini kuhusu masuala ya Qur'ani, kidini na kiitikadi, alibainisha.
Baraza la Sayansi ya Qur'ani, lenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram ya Hazrat Abbas (AS) linaandaa programu mbalimbali za kidini na Qur'ani kwa ajili ya wafanyaziara wanaozuru maeneo matakatifu nchini Iraq katika hafla za kidini.
4234625