IQNA

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah

Iran, nchi pekee inayounga mkono ukombozi wa Palestina

13:06 - July 11, 2015
Habari ID: 3326617
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema Iran ndio nchi pekee inayounga mkono ukombozi wa ardhi zote za Palestina na Quds Tukufu.

Nasrullah alitoa tamko hilo katika hotuba yake jana Ijumaa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds.
Sayyid Nasrullah amesema Iran ndio nchi pekee ambayo kwa mtazamo wa watawala wa Israel, ni tishio kwa utawala huo na kwa msingi huo Wazayuni wanaeneza chuki kote duniani dhidi ya Iran. Kiongozi huyo wa Hizbullah amesema licha ya kuwekewa vikwazo, kutishiwa kuvamiwa kijeshi na kukumbwa na vita vya kisaikolojia, Iran ndio nchi pekee inayounga mkono Palestina. Nasrullah amesema kuiunga mkono Palestina ni kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba uadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni uadui dhidi ya Palestina.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema 'Israel ni mama wa ugaidi wote' na kwamba utawala wa Israel unahadaa walimwengu unapodai kupambana na ugaidi. Sayyid Nasrullah amesisitiza kuwa, baada ya Syria kutumbukia katika vita, maadui walielekeza nguvu zao upande wa Iran na Hizbullah kama tishio kubwa zaidi. Amesema Hizbullah ina fahari kuwa imegeuka na kuwa tishio la kistratijia kwa Israel.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa harakati hiyo itaendelea kuunga mkono mapambano ya Syria dhidi ya ugaidi huku akisisitiza kuwa serikali ya Syria ikianguka Palestina pia itaanguka.
Katika hotuba yake hiyo mjini Beirut, Sayyid Nasrullah pia ameashiria hujuma ya jeshi la Saudia dhidi ya watu wa Yemen na kusema, Waarabu Waislamu wamewasahau Wayemen.  Amesema, "Vita dhidi ya Yemen ni huduma kubwa zaidi ya Saudi Arabia kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.".../mh

3326304

captcha