IQNA

Tamasha la Kimataifa la Qur’ani Moscow kwa mara ya kwanza

15:24 - July 13, 2015
Habari ID: 3327667
Tamasha la Kimataifa ya Qur’ani linafanyika Moscow mji mkuu wa Russia kwa mara ya kwanza kabisa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Russia TASS, tamasha hilo linafanyika kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yalianza Julai 11.
Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mamufti wa Russia Rushan Abbyasov amesema tamasha hilo litafanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Moscow kwa muda wa siku saba.
Wanazuoni wa kidini, watarjumi, wakiwemo  kutoka Iran, Jamhuri ya Azerbaijan, Kazakhstan, Tajikistan, Uturuki na India wanatazamia kuhutubia tamasha hilo.
Washiriki wataonyesha kazi zao  za Kiislamu kuhusu Qur’ani Tukufu, filamu, habari, fasihi ya kisayansi, vitabu vya wanazuoni wa Kiislamu na vitabu vilivyotarjumiwa..../mh

3326356

captcha