IQNA

Waislamu Russia

Maonyesho ya Maonyesho ya 'Ulimwengu wa Qur'ani' yafanyika Moscow

16:14 - November 10, 2024
Habari ID: 3479729
IQNA - Maonyesho ya 'Ulimwengu wa Qur'ani' yamefunguliwa katika mji mkuu wa Russia siku ya Jumamosi.

Msikiti wa Jamia Moscow ndio mwenyeji wa maonyesho hayo, ambayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Qatar.
Kwa mujibu wa Rushan Abbyasov, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mamufti Russia, wageni wanaweza kujifunza kuhusu hali ya miji mitakatifu ya Makka na Madina wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (SAW).
Alisema pia kuna programu maalum kwa watoto na watu wazima katika maonyesho hayo.
Ameongeza kuwa kongamano la kimataifa na wiki ya sinema za Kiislamu pia zimeandaliwa katika Msikiti wa Jamia Moscow pamoja na maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yalizinduliwa siku moja baada ya kumalizika kwa Mashindano ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Moscow.
Yamhudhuriwa na wahifadhi Qur'ani kutoka zaidi ya nchi 30, zikiwemo nchi 9 za Afrika.
Russia ni nchi kubwa yenye watu milioni 146. Uislamu ni dini ya wachache nchini Russia ambapo kuna takriban Waislamu milioni 25. Nchi hiyo ina Waislamu wengi zaidi barani Ulaya.
Watu wengi wa Urusi ni Wakristo wa Orthodox. 

4247182  

 

Kishikizo: russia waislamu
captcha