"Kamwe hatutaunga mkono marufuku ya hijabu kwa kisingizio chochote kila," amesema Khalid Aliyu Abubakar, Katibu Mkuu wa JNI.
Kwa mujibu wa Abubakr, sera ya kuwanyoshea kidole na kuwatuhumu wanawake Waislamu wanaovaa hijabu, katika fremu ya sera za serikali kupambanan na ugaidi, ni sawa nia ubaguzi kwa msingi wa kidini.
Katika wiki za hivi karibuni magaidi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram huko Nigeria wamekuwa wakiwatumia magaidi wa kike kutekeleza hujuma za kigaidi. Kufuatia hali hiyo, serikali ya Nigeria sasa inawafanyia upekekuzi mkali wanawake Waislamu wanaovaa Hijabu.
Abubakr amesema JNI inapinga hatua ya vyombo vya usalama kuwafanyia upekuzi 'wanawake wote Waislamu' na kusema upekuzi huo unapaswa kufanyika wakati tu kuna shaka ya hali ya juu. Ameongeza kuwa hatua kama hizo za kibaguzi si tu kuwa ni za kibaguzi bali pia hazifikii lengo la kuangamiza ugaidi.
"Hijabu inalaumiwa kana kwamba hijabu yenyewe inatekeleza ugaidi," amesema. Ametaka vyombo vya usalama Nigeria kukabiliana na ugaidi kwa kutumia mbinu za kisasa za uchunguzi.../mh