Ofisi hiyo imetoa taarifa na kusema kuwa, Alhamisi jioni mwezi mwandamo haukuonekana na kwa msingi huo Ijumaa hii ni siku ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na keshi, ni Idul Fitr, Inshaallah.
Serikali ya Oman pia imetangaza kuwa mwezi haukuandamana jana Alkhamisi na kwa hivyo Idul Fitr itaadhimishwa kesho nchini humo. Afghanistan na Morocco pia ni kati ya nchi ambazo Idul Fitr itaadhimishwa kesho. Pamoja na hayo baadhi ya nchi kama vile Syria, Saudi Arabia, Misri, Qatar na Indonesia zimetangaza Ijumaa ya leo kuwa ni Idul Fitr.
Nchini Kenya Kadhi Mkuu Sheikh Ahmed Muhdhar jana Alkhamisi pia alitangaza kuwa Waislamu nchini wataadhimisha Idul Fitr Siku ya Jumamosi. Akizungumza mjini Mombasa, amesema mwezi haukuandamana eneo la pwani kama ambavyo pia haujaandamana maeneo mengine ya Afrika Mashariki hasa Tanzania na Zanzibar.../mh