IQNA

Zaidi ya Waislamu laki moja waliuawa vitani, katika maafa mwaka 2014

20:28 - August 18, 2015
Habari ID: 3345845
Waislamu wasiopungua 108,000 walipoteza maisha kutokana na maafa na vita katika nchi za Kiislamu na nchi ambazo Waislamu ni wachache kote duniani mwaka 2014.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya Misaada ya Kibinaadamu katika Shirika la Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (ICHAD-OIC). Ripoti hiyo imebaini kuwa kuna migogoro na maafa 45 katika nchi 27 zikiwemo nchi za OIC na nchi ambazo Waislamu ni wachache kama vile Myanmar na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ripoti hiyo imezitaja nchi za OIC ambazo zinakumbwa na migogoro na vita kuwa ni pamoja na Iraq, Syria, Yemen, Libya, Afghanistan na Somalia kati ya nyinginezo. Katibu Mkuu wa OIC Iyad Madani amesema hali ya kibinadamu imezorota sana katika nchi hizo kutokana na malumbano ya kisiasa. Amesema OIC inajitahidi kuanzisha mbinu za kuzisaidia nchi wanachama kuzuia migogoro na vita. Ripoti hiyo imesema mwaka 2014 Syria ilishuhudia idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza maisha ambapo kulikuwa na vifo 67,021 ikifuatiwa na Iraq ambapo watu 15,538 walipoteza maisha, Nigeria watu 8,464 na Afghanistan watu 4,950 waliuawa. Ripoti hiyo imesema Wapalestaina 2,081 waliuawa shahidi kutokana na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza, huku nchini Yemen watu 1500 na Libya watu 600 wakiuawa katika mapigano ya ndani ya nchi. Sierra Leone and Guinea nazo zilishuhudia idadi kubwa ya Waislamu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kuambukiza wa Ebola.../mh

3345484

captcha