Katika ujumbe maalumu aliotoa jana Ali Larijani, mbali na kutoa salamu za rambirambi kwa Waislamu kufuatia tukio la kusikitisha la Makka alitoa mkono wa pole pia kwa familia za mahujaji waliopoteza maisha na kueleza kwamba serikali ya Saudia ilipaswa ichukue hatua za lazima kuhakikisha usalama wa mahujaji, lakini uzembe iliofanya umesababisha kutokea tukio hilo. Spika wa bunge la Iran ameeleza katika ujumbe wake huo kwamba maafa hayo ya kusikitisha yamezitonesha na kuziungulisha nyoyo za umma wa Kiislamu na kuichanganya Hijja ya Kiibrahim na simanzi na majonzi na kwamba kuna udharura wa kufanyika uchunguzi unaohitajika juu ya tukio hilo. Watu wasiopungua 107 walifariki dunia na wengine wasiopungua 238 walijeruhiwa siku ya Ijumaa baada ya winchi au kreni kuangukia msikiti mtukufu wa Makka.