IQNA

Kiongozi wa Ansarullah

Njama za kudhoofisha umma wa Kiislamu

14:31 - October 25, 2015
Habari ID: 3393529
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah nchini Yemen amesema watawala madhalimu wanapanga njama za kudhoofisha umma wa Kiislamu kwa kuuweka mbali na thamani za misingi ya haki.

Sayyid Abdulmalik Badruddin Houthi, Katibu Mkuu wa Ansarullah ameyasema hayo Jumamosi kwa mnasaba wa Siku ya Ashura katika mji mkuu wa Yemen, Sana’a. Akiwahutubia waombolezaji wa Imam Hussein AS, amesema watenda jinai wanatekeleza njama za kubadilisha mwelekeo wa Waislamu na wapenda haki kwa kupotosha dini na kuonyesha vigezo visivyo vya kweli.

Abdulmalik Badruddin amesema Waislamu wote na wapenda uhuru katika jamii za Kiislamu wana jukumu la kuangamiza tatizo hili kubwa ambalo limeyasababishia masaibu mataifa ya eneo. Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema umoja wa Waislamu ni muhimu katika kukabiliana na watenda jinai katika eneo. Aidha amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umetenda jinai mbaya zaidi dhidi ya taifa la Palestina. Katika sehemu nyengine ya hotuba yake Kiongozi wa Ansarullah amesema Wayemen wana azma imara ya kukabiliana na hujuma ya kinyama ya Saudia dhidi ya nchi yao. Aidha amefichua kuwa hujuma ya Saudia dhidi ya Yemen imefanyika kwa uchochezi wa Israel na Marekani.../mh

3393142

captcha