IQNA

Waislamu Marekani wamlaani Trump kwa kueneza chuki dhidi ya Waislamu

12:52 - December 08, 2015
Habari ID: 3461178
Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani CAIR limemlaani Donald Trump anayewania kuteuliwa kugombea urais wa tikiti ya chama cha Republican, kufuatia matamshi yake kuwa Waislamu watimuliwe Marekani.

CAIR imesema matamshi ya Trump yanakiuka katiba na kwamba mwanasiasa huyo anaeneza aina mbaya zaidi ya chuki dhidi ya Uislamu.
Trump amenukuliwa akitaka serikali ya Barack Obama kutoruhusu wahajiri Waislamu kuingia nchini humo bila ya kujali wanatokea nchi gani.
Amedai kuwa serikali ya Barack Obama haijui nini kinaendelea hivi sasa na inapaswa kuangalia itikadi za kidini za watu na kuzuia Waislamu kukanyaga ardhi ya Marekani.
Ameongeza kuwa, uchunguzi wa taasisi za kukusanya maoni ya watu unaonesha kuwa, jamii za Waislamu kote duniani zina mtazamo wa chuki kuhusiana na Marekani na hata baadhi ya Waislamu wanaendesha kampeni za kutumia nguvu kupambana na Marekani.
Hata hivyo Ikulu ya Marekani White House imejibu haraka madai hayo kwa kusema, matamshi ya namna hiyo yanapaswa kulaaniwa kwani yanakinzana na manufaa ya Marekani kwani hayahubiri vita kati ya Marekani na ugaidi, bali yanachochea vita kati ya Marekani na dini ya Kiislamu.

3461041

Kishikizo: marekani trump waislamu
captcha