Rais wa Iran na Papa Francis wamesisitiza umuhimu wa kushadidishwa vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali. Papa amezungumzia matatizo yanayolikabili eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa, Iran ni nchi yenye nafasi ya kipekee katika eneo hilo na kwa mantiki hiyo inapaswa kushirikishwa katika michakato yote ya kutatua matatizo ya kieneo.
Kabla ya kuonana na Papa Francis huko Vatican, Rais Rouhani alikutana na Waziri Mkuu Matteo Renzi na Rais Sergio Mattarella mjini Rome, Italia.
Wakati huo huo masanamu yote uchi ya Jumba la Makumbusho la Capitoline katika mji mkuu wa Italia, Roma yamefunikwa wakati wa mkutano wa Rais Hassan Rouhani na Waziri Mkii wa Italia, Matteo Renzi.
Msemaji wa jiji la Roma amesema uamuzi wa kufunikwa masanamu yote uchi ya Jumba la Makumbusho la Capitoline kwa heshima ya Rais Rouhani ulichukuliwa na ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Shirika la habari la Italia, ANSA limeripoti kuwa masanamu ya jumba hilo la makumbusho yamefunikwa kwa heshima ya Rais wa Iran anayeitembelea Italia. Vilevile vileo na mvinyo havikuwekwa katika meza ya karamu ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Waziri Mkuu wa Italia kwa ajili ya Rais Hassan Rouhani na ujumbe unaoandamana naye ikiwa ni kuoneesha heshima kwa maadili na sheria za Kiislamu.
3458895