IQNA

Rais wa Iran akimpokea Balozi wa Vatican

Mazingatio kwa Mola Muumba na umanaawi udharura kwa jamii ya mwanadamu

16:28 - November 23, 2021
Habari ID: 3474593
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kutoa mazingatio kwa Mola Muumba na suala la umanaawi ni jambo la udharura mkubwa hii leo kwa jamii ya mwanadamu.

Rais Sayyid Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo Jumanne wakati akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Andeji Yusovic Balozi Mpya wa Vatican hapa Tehran. Rais wa Iran amesisitiza kwamba, ni jambo la dharura hii leo kwa jamii ya mwanadamu kutoa mazingatio kwa Mola Muumba na suala la umaanawi. Halikadhalika amesema kwamba kwa mujibu wa mafundisho ya Qur'ani,  nukta zinazotukutanisha pamoja ni dini  za Nabii Ibrahim AS ambazo zinaagiza kuwepo umoja na mshikamano kati yetu.

Ameongeza kuwa wale wanaodhulumu na kufanya ukandamizaji duniani hii leo kama wangezingatia mafundisho ya Nabii Isa Masih AS wasingeweza kutenda dhulma hizo; na Vatican inaweza kuwa na nafasi na mchango muhimu katika uwanja huo.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, mafundisho ya dini ya Ukristo na kile alichotufunza Mtume Mtukufu wa Uislamu SAW yanapasa kujadiliwa katika vikao vya kielimu ili kukurubisha zaidi mitazamo baina yetu.  

4015670

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha