Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Muhammad Javad Zarif amesema Waislamu wanapaswa kuungana ili kuonyesha nchi za Magharibi kuwa wanaweza kupambana na ugaidi na misimamo mikali ya kidini.
Zarif ameyasema hayo Jumanne usiku mjini Paris Ufaransa na kuongeza kuwa, ugaidi umeathiri vibaya Waislamu na nchi za Kiislamu duniani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amebaini kuwa, badala ya Waislamu kuchochea tafauti baina yao, wanapaswa kuoneysha namna ya kukabiliana na changamoto zinazoukumba Uislamu na pia washirikiane katika kustawisha mataifa ya Kiislamu na jamii za Waislamu kote duniani.