IQNA

Kongamano la Masomo ya Qur'ani lafanyika Manchester, Uingereza

18:42 - July 18, 2016
Habari ID: 3470463
Kongamano la Kimataifa kuhusu masomo ya Qur'ani Tukufu limemalizika katika mji wa Manchester nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo lilolikuwa na kaulimbiu ya "Masomo ya Qur'ani na Kutafakari Kuhusu Qur'ani Barani Ulaya" lilianza Ijumaa 15 Julai na kumalizika Jumapili 17 Julai.

Kongamano hilo liliandaliwa na Akademia ya Sayansi za Qur'ani Ulaya kwa ushirikiano na Kituo cha Turathi za Waislamu mjini Manchester pamoja na Taasisi ya Qur'ani ya Tibyan.

Maudhui kuu katika kongamano hilo ilikuwa ni, "Uadilifu na Ukarimu katika Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Mtukufu SAW."

Makala zilizowasilishwa katika kogamano hilo zilijadili mada kama vile uhuru katika Uislamu, uadilifu katika aya za mirathi za Qur'ani Tukufu n.k.

Kongamano hilo limefanyika kwa lengo la kuarifisha mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kuwahimiza Waislamu kutafakari (tadabbur) na kufanya utafiti kuhusu maudhui mbali mbali za Qur'ani Tukufu

captcha