IQNA

Saudia yadondosha mabomu misikitini Yemen

10:09 - August 09, 2016
Habari ID: 3470511
Ndege za kivita za Saudi Arabia zimedondosha mabomu katika msikiti mwingine huko kaskazini mashariki mwa Yemen.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, siku ya Jumatatu, ndege za kivita za Saudia zilidondosha mabomu katika msikiti ulio katika wilaya ya Dwar mjini Mostaba, katika mkoa wa Hajjah kaskazini mashariki mwa Yemen.

Picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zimeonyesha msikiti huo ukiwa umeharibiwa vibaya kufuatia hujuma hiyo ya ndege za kivita za Saudia.

Mapema Jumatatu, msikiti mwingine ulidondoshewa mabomu na ndege za kivita za Saudia katika wilaya ya Al Ammar mjini al Safra. Duru zinasema msikiti huo uliharibiwa kabisa katika hujuma hiyo ya ndege za kivita za Saudia.

Maelfu ya Wayemeni wakiwemo wanawake na watoto wameuliwa na kujeruhiwa na makumi ya maelfu wamekuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Saudi Arabia na waitifaki wake ambao walianza kuihujumu Yemen kinyemye cha sharia Machi 2015. Mbali na hayo, asilimia 80 ya miundombinu, huduma za kijamii na kitiba zimeharibiwa na kubomolewa katika uvamizi huo wa kijeshi wa utawala wa Aal Saud dhidi ya Yemen.

Saudi Arabia ilianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen tangu mwanzoni mwa mwaka jana chini ya muungano unaozishirikisha baadhi ya nchi za Kiarabu za eneo kwa kuungwa mkono na Marekani, lengo kuu likiwa ni kumrejesha madarakani Rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu Abd Rabu Mansour Hadi na ili kuwazuia kushika madaraka wanamapinduzi wa nchi hiyo ambao wanadhamini usalama wa miji ya nchi hiyo.

3460642

captcha