Amehukua nafasi ya Sheikh Shawki Allam ambaye alihudumu katika nafasi hiyo kwa takriban miaka kumi. Uteuzi huo ulitokana na mapendekezo kutoka kwa Sheikhe Mkuu wa Al-Azhar Sheikh Ahmed El-Tayyeb.
Sheikh Ayyad ana shahda ya Uzamivu, PhD, katika imani na falsafa ya Kiislamu na ameandika zaidi ya vitabu 30 katika fani hizo.
Anajulikana kama mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar katika nyanja za Fiqh (sheria za Kiislamu), imani na falsafa ya Kiislamu.
Anajulikana pia kwa mtazamo wake wa wastani na juhudi zake za kukuza mazungumzo ya dini tofauti na kukabiliana na itikadi kali, chuki dhidi ya Uislamu na upotovu wa itikadi ya takifiri au ukufurishaji..
Hapo awali Sheikh Ayyad aliwahi kuwa katibu mkuu wa Chuo cha Utafiti cha Kiislamu cha Al-Azhar. Ayyad alipata digrii yake ya kwanza katika Misingi ya Dini, alibobea katika Imani na Falsafa mnamo 1995. Baadaye, alipata digrii ya uzamili katika fani hiyo hiyo mnamo 2000 na akamaliza PhD yake ambapo alipata daraja la kwanza mnamo 2003.
Sheikh Ayyad alianza maisha yake ya kitaaluma kama msaidizi wa kufundisha na akaendelea na kuwa mhadhiri msaidizi, kisha mhadhiri, na hatimaye profesa msaidizi katika Kitivo cha Misingi ya Dini huko Mansoura.
Baada ya hapo, alijiunga na wafanyikazi wa Kitivo cha Mafunzo ya Kiislamu na Kiarabu kwa Wasichana huko Kafr El-Sheikh kama profesa msaidizi katika Idara ya Imani na Falsafa, na kisha profesa kamili mnamo 2016.
3489485