IQNA

15:13 - May 28, 2018
News ID: 3471535
TEHRAN (IQNA)- Mashidano ya Kimataifa ya 19 ya Kuhifadhi Qur'ani ya Tazania yamefanyija Jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo Dar-es-Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa, hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Tanzania, Shujaa Suleiman Shujaa, ametangazwa mshindi na kutunukiwa zawadi ya shilingi za Tanzania milioni 15. Halikadhalika amepata zawadi ya laptop na kipande cha ardhi mjini hapo.

Akihutubu katika mashindano hayo ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Taifa jini Dar-es-Salaam, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alitoa wito kwa Watazania kudumisha amaani iliyopo katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki huku akisisitiza kuwa, kama hakutakuwa na amani basi watu hawataweza kufanya ibada.

Katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na washiriki kutoka nchi 18, mshindi wa pili alikuwa ni Ahmed Noor wa Sudan aliyetunukiwa zawadi ya Shilingi milioni 12 pamoja na laptop akifuatiwa na Muzzamil Awadh pia wa Sudan ambaye alipata zawadi ya shilingi milioni 7.5. Nafasi ya nne ilichukuliwa na Abdulally A. Mohamed wa Kenya  ambaye alitutunukiwa zawadi ya shilingi milioni 5.7 huku Ibrahim Maazuri wa Niger akishika nafasi ya tano na kutunukiwa zawadi ya shilingi milioni 3. Saudia imewapa washindi watano tiketi za kushiriki katika Ibada ya Hija.

Baadhi ya nchi zingine zilishoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Burundi, Djibouti, Ethiopia, Nigeria, Ghana Msumbuji na Visiwa vya Komoro.

 Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tanzania yafanyika

 

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tanzania yafanyika

3718251

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: