IQNA

Waislamu zaidi ya milioni mbili Waswali Makka, Madina Usiku wa Laylatul Qadr

10:14 - June 13, 2018
Habari ID: 3471556
TEHRAN (IQNA)- Waislamu zaidi ya milioni mbili walifurika katika Msikiti Mkuu wa Makka (al-Masjid al-Haram) na Msikiti wa Mtume SAW (al-Masjid an-Nabawi) mjini Madina Jumatatu.

Waislamu walikusanyika katika misikiti hiyo miwili mitakatifu zaidi katika Uislamu kwa munasaba wa usiku wa 27 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao kwa mujibu wa Riwaya za Ahul Sunna unaaminika kuwa wenye uwezekano mkubwa sana kuwa usiku  wa cheo au Laylatul Qadr kati ya nyusiku 10 za mwisho za Mwezi wa Ramadhani.

Kwa mujbu wa vyombo vya habari vya Saudia, waumini wenye matumaini ya kupata baraka na rehema za Allah na kusamehewa madhambi yao walimininika katika misikiti hiyo miwili kuanzia wakati wa Sala ya Ishaa iliyofuatiwa na sala ya Tarawih na kisha sala ya usiku wa manane inayojulikana kama Qiyamullail.

Kwingineko vyombo vya habari vya Palestine vimeripoti kuwa Jumatatu Wapalestina zaidi ya 250,000 walihuisha usiku wa Laylatul Qadri katika msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Wapalestina walimimnika katika msikiti huo ambao ni sehemu ya tatu kwa utukufu katika Uislamu pamoja na kuwepo vizingiti vikali vilivyokuwa vimewekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Wazayuni waliwazuia Wapalestina isipokuwa wale wenye umri wa chini ya miaka 40 kuswali katika Msikiti wa Al Aqsa.

3722196/

captcha