IQNA

Mpango wa usimamizI wa Mwezi wa Ramadhani Umezinduliwa Makka

17:20 - February 26, 2025
Habari ID: 3480270
IQNA – Mpango wa usimamizi wa mwezi mtukufu wa Ramadhan umezinduliwa katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Sheikh Abdulrahman Al-Sudais, mkuu wa Idara ya Dini katika Msikiti Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram)  na Msikiti wa Mtume (al-Masjid an-Nabawi) , alizindua mpango huo.

Unalenga kuongeza umuhimu wa kiroho wa mwezi mtukufu kwa kusisitiza fadhila zake na kuimarisha hadhi takatifu ya Msikiti Mkuu wa Makka, kulingana na Shirika la Habari la Saudi.

Unalenga kuwalisha mazingira bora ya kidini kwa wageni na mahujaji wa Umrah kupitia huduma za hali ya juu na mipango bunifu.

Sheikh Al-Sudais alisema kuwa mpango huo unajumuisha mfululizo wa mipango inayolenga kuongeza ushiriki wa kidini na kitamaduni wa waumini.

Zaidi ya programu 120 za kisayansi, kifikra na mwongozo zimeanzishwa ili kuimarisha ufahamu wa wageni juu ya thamani ya kiroho ya Ramadan.

Mpango huo pia unajumuisha njia 10 za kuboresha uzoefu wa wale wanaotembelea Miji Miwili Mitakatifu wakati wa mwezi mtukufu.

3492027

Habari zinazohusiana
Kishikizo: makka ramadhani
captcha