IQNA

Kiongozi wa Hizbullah katika Majlis ya Muharram
11:06 - September 20, 2018
News ID: 3471680
TEHRAN (IQNA) Kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ndiyo inayorefusha uwepo wa baadhi ya mabaki ya magaidi wa ISIS au Daesh katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mashariki mwa Syria.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema hayo usiku wa kuamkia leo kwa mnasaba wa mwezi kumi Muharram, (usiku wa Ashura) na kuongeza kuwa Marekani inataka magaidi wa ISIS waendelee kuweko Syria ili iendelee kuhalalisha uwepo wa majeshi yake vamizi katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Kiongozi wa Hizbullah ameendelea kusema kuwa, hivi sasa magaidi wa ISIS wanahamishiwa Afghanistan, Pakistan, Misri na Yemen baada ya kusambaratishwa huko Iraq na Syria.

Aidha amewakosoa vikali baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu na kusema mabalozi wa Marekani ndio watawala halisi wa baadhi ya nchi za Kiarabu.

Kwingineko katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, hujuam za utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Syria hazitavumilika tena na hatua zinapaswa kuchukuliwa kukomesha uchokozi huo wa kila uchao. Amesema, mashambulizi ya Israel huko Syria yana mfungamano wa moja kwa moja na kushindwa njama za mhimili wa Marekani - Saudia – Israel. Amebaini kuwa pigo hilo ndilo ambalo limeupelekea ndio utawala wa Kizayuni utekeleza kila aina ya njama kuizuia Syria kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa makombora ya kijihami.

3748434

Name:
Email:
* Comment: