IQNA

Mamillioni wafika katika mjumuiko mkubwa zaidi wa kidini duniani mjini Karbala

22:17 - October 18, 2019
Habari ID: 3472177
TEHRAN (IQNA) - Mamilioni ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanakusanyika katika mji mtakatifu wa Karbaka nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya Arubaini ya Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS.

Wafanyaziara takribani milioni 20 kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wameelekea Karbala kwa miguu baada ya kukata masafa ya karibu kilomita 80 kutoka katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq. Wengi kati ya washiriki katika mjumuiko huo waliwasili katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala wiki moja kabla, wakijitayarisha kwa ajili ya marasimu na shughuli ya Arubaini ya Imam Hussein inayomaanisha siku ya Arubaini baada ya tarehe 10 Muharram, siku aliyouawa shahidi mjukuu huyo wa Mtume wa Muhammad SAW. Mwaka huu tarehe 20 Safar ambayo ni siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS inasadifiana na 19 Oktoba.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Abdolreza Rahmani Fazli amesema kuwa, Wairani milioni 3.5 wameingia Iraq kwa ajili ya kushiriki katika shughuli ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Mamilioni ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu kutoka nchi nyingine za kigeni pia wamewasili Karbala kwa ajili ya kushiriki katika shughuli hiyo hususan kutoka nchi za Pakistan, Afghanistan, Azerbaijan, Uturuki, india, Kuwait, Bahrain na Lebanon. Aidha kuna washiriki kutoka nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Madagascar. Aidha kuna idadi kubwa wa wageni kutoka nchi za Ulaya na Marekani.

Wanoshiriki katika matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS wanakaribiswa kwa ukarimu mkubwa na watu wa Iraq ambao wanawahudumia kwa kuwapa makazi, chakula, usafiri na huduma nyingine muhimu.

Mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as) aliuawa shahidi mwaka 61 Hijria katika ardhi ya Karbala nchini Iraq akiwa pamoja na familia na masahaba zake 72 wakipambana dhidi ya dhulma na upotoshaji uliokuwa ukifanywa na mtawala wa wakati huo Yazid bin Muawiya katika mafundisho ya dini ya Uislamu.

Historia inasema mtu wa kwanza kuzuru kaburi la mtukufu huyo alikuwa Sahaba wa Mtume Muhammad (saw) Jabir bin Abdillah al Ansari ambaye alifika Karbala na kwenye kaburi la Imam Hussein katika siku ya arubaini tangu baada ya mauaji yake.

Imam Husain AS aliuawa shahidi kikatili na kinyama tarehe 10 Muharram mwaka wa 61 Hijria, yaani miaka 1380 iliyopita, katika jangwa la Karbala, Iraq ya leo, akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kuongoza mapambano ya kishujaa ya ushindi wa damu mbele ya upanga.

Vita vya Karbala vilikuwa moja kati ya vita mashuhuri katika historia ya Kiislamu na ya mwanadamu, vilitokea baina ya majeshi ya haki na batili katika ardhi ya Karbala huko Iraq. Siku aliyouawa shahidi Imam Hussein AS inajulikana kwa jina la Ashura.

3469686

captcha