IQNA

Muqawama

Mchambuzi wa Iraq: Shahidi Soleimani alikuwa Sauti ya Umoja na Haki

22:01 - January 04, 2025
Habari ID: 3480004
IQNA – Luteni Jenerali Qassem Soleimani alikuwa sauti ya umoja na haki, na hili limemfanya kuwa nembo ya milele katika fahamu za mataifa ya eneo la Asia Magharibi, amesema mchambuzi wa kisiasa wa Iraq.

 

Akizungumza na IQNA katika kumbukumbu ya miaka 5 ya kuuawa shahidi kwa Jenerali Soleimani, Salah al-Zubaidi alisema jenerali huyo mwandamizi wa Iran hakuwa kamanda wa kijeshi tu, bali alikuwa mradi wa umoja wa ustaarabu.

"Aliweza kuvuka tofauti za kidini na kikabila na kuzingatia lengo la umoja katika kukabiliana na nguvu za kibeberu za kimataifa."

Jenerali Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (PMU), pamoja na baadhi ya wenzao, waliuawa kwa shambulio la kigaidi landege isiyo na rubani la Marekani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mnamo Januari 3, 2020.

Al-Zubaidi alisema kuwa utu kamili wa Shahidi Soleimani na mtazamo wake wa kina ulimfanya kuwa ishara na nembo ya mhimili wa muqawama, akivutia makundi na vikosi mbalimbali vya muqawam katika eneo.

Aliongeza kuwa Mashahidi Soleimani na al-Muhandis walijitolea maisha yao kutetea uhuru, utulivu na amani ya Iraq, na kuwa nembo za ujasiri na kujitolea.

"Wakiwa wamesimama pamoja dhidi ya ugaidi, walitetea masuala ya umma wa Kiislamu, hivyo kuonyesha roho ya udugu wa Kiislamu katika namna yake nzuri zaidi."

Mashahidi hawa wawili walikuwa na lengo moja, nalo lilikuwa ni uhuru wa Iraq na kuhifadhi heshima ya taifa la Iraq, alisema, akiongeza kuwa damu yao safi inatoa ujumbe wazi kuwa njia ya uhuru na uhuru inajengwa na kujitolea na kuuawa shahidi.

Alisema jukumu lao halikuwa tu la kijeshi bali pia lilihusisha kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa ya eneo hilo na vikosi vya kitaifa.

"Hii ilichangia sana katika kutokomeza ugaidi na kurejesha usalama kwa mataifa yaliyoathirika na uharibifu wa vita."

3491316

Habari zinazohusiana
Kishikizo: Qassem Soleimani
captcha