IQNA

10:39 - February 07, 2020
News ID: 3472446
TEHRAN (IQNA) - Waziri Kiongozi wa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na Pakistan amesema kuwa upatanishi wa Marekani katika utatuzi wa mzozo wa eneo hilo hautakuwa na maslahi kwa Waislamu huku Siku ya Kashmir ikiadhimishwa kote duniani.

Akizungumza kwa mnasaba wa kushikamana na watu wa Kashmir inayodhibitiwa na India, ambayo huadhimishwa Februari 5,  Farooq Haider Khan amesema kuwa kuingia Marekani katika suala la Kashmir ni hatari kubwa. Waziri Kiongozi huyo ameongeza kwamba Marekani kamwe haiwezi kuingia katika mzozo huo kwa maslahi ya Wakashmir wala Waislamu na kuwa uamuzi wowote itakaouchukua kuhusiana na eneo hilo bila shaka utakuwa kwa maslahi ya Wahindi.

Matamshi ya Waziri Kiongozi huyo wa Kashmir kuhusu juhudi za Marekani za kuingilia masuala ya eneo hilo kwa kisingizio cha upatanishi yanatokana na uzoefu hasi wa nchi hiyo katika upatanishi wake wa upendeleo katika migogoro mbalimbali ya kieneo na kimataifa. Mfano wa wazi wa suala hilo ni mpango wa kidhalimu uliozinduliwa hivi karibuni na Marekani kuhusiana na mzozo wa muda mrefu zaidi katika eneo la Asia Magharibi, kwa jina la 'Muamala wa Karne' ambapo imeonyesha upendeleo wa wazi kwa utawala ghasibu wa Israel kwa madhara ya Waislamu wa Palestina.

Kwa kutilia maanani kwamba serikali yenye hila na hadaa ya Marekani kupitia mpango huo wa kishetani unaoitwa 'Muamala wa Karne', imekanyaga haki zote za Waislamu na taifa dhulumiwa la Palestina huku ikiteteta kwa hali na mali maslahi haramu ya utawala ghasibu wa Israel unaoendelea kuua kikatili watoto na wanawake wa Kipalestina, rekodi ya White House katika kueneza dhulma na kukanyaga haki za Waislamu ni jambo linaloonekana wazi mbele ya walimwengu.

Ni kutokana na ukweli huo ndipo, Waziri Kiongozi wa Kshmir inayodhibitiwa na Pakistan akasema wazi kuwa uingiliaji wa Marekani katika utatuzi wa mgogoro wa Kashmir inayodhibitiwa na India bila shaka utakuwa kwa maslahi ya serikali ya New Delhi na kwa madhara ya moja kwa moja ya watu wa Kashmir.

Kwa kutilia maanani ushirikiano wa kistratijia wa Marekani na India na hasa baada ya kutiwa saini mkataba wa ushirikiano wa pande hizo katika uwanja wa nyuklia katika kipindi cha uongozi wa Barack Obama, Rais wa zamani wa Marekani, ni wazi kuwa ingiliaji wa White House katika mzozo wa Kashmir utakuwa tu kwa madhara ya watu wa eneo hilo.

Mnamo mwaka 1947 India na Pakistani zilipopata uhuru maeneo yaliyokuiwa na Waislamu wengi yalikabidhiwa chini ya Pakistani huku yale yaliyokuwa na wahindu wengi yalikabidhiwa chini ya India. Kwa upande wa Kashmir ambayo asilimia 90 ya wakaazi wake ni waislamu, Mkoloni Muingereza haikuikabidhi chini ya Pakistani. Hivi karibuni

Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan amesisitizia ulazima wa kufanyika kura ya maoni katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India. Huku akitangaza uungaji mkono wake wa kila upande kwa Waislamu wanaoishi eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India amesema kuwa, umefika wakati kwa serikali ya New Delhi kuheshimu takwa la Umoja wa Mataifa juu ya kufanyika kura ya maoni katika eneo hilo.

3470555

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: