IQNA

Hujuma ya India imeua watu 13 msikitini nchini Pakistan

22:16 - May 07, 2025
Habari ID: 3480652
IQNA- Watu 13 Wauawa Katika Shambulio la India Kwenye Msikiti wa Pakistan: Afisa Shambulio la kombora la India kwenye msikiti huko Bahawalpur, mji katika Punjab ya Pakistan, afisa wa Pakistani alisema. Afisa huyo aliongeza kuwa wanawake na watoto walikuwa miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo.

India iilifyatua makombora kadhaa ndani ya ardhi ya Pakistan mapema leo alfajiri na kusababisha vifo vya raia wasiopungua 26, katika mashambulizi yanayoweza kuzusha vita baina ya nchi hizo mbili jirani na hasimu wa miaka mingi. India nayo imedai kuwa mizinga ya Pakistan imeua watu 10 katika mpaka wa nchi hizo mbili.

Mamlaka za Pakistan zimesema makombora ya India yalililenga jimbo linalozozaniwa na pande hizo mbili la Kashmir pamoja na mkoa wa mashariki wa Punjab. Moja ya makombora lilimepiga msikiti kwenye mji wa Bahawalpur na kuua mtoto mmoja na kujeruhiwa watu wengine kadhaa.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif amelaani mashambulizi hayo ya anga na kusema nchi yake inayo haki ya kulipa kisasi kwa hujuma hizo za India alizozitaja kuwa "kitendo cha kivita".

Pakistan imesema imefanikiwa kutungua ndege tano za Jeshi la Anga la India na ndege moja isiyo na rubani katika hatua ya “kujilinda.” Pakistan imesema kwamba ndege za kisasa za Rafale zilizotengenezwa Ufaransa  zilikuwa miongoni mwa ndege za kivita zilizoangushwa pamoja na MiG-29 na SU-30.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake kuhusu operesheni za kijeshi zinazofanywa na jeshi la India kwenye mstari wa usimamizi na mpaka wake wa kimataifa na Pakistan.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa na Msemaji wa Umoja wa Mataifa  jioni ya Jumanne Mei 6 kwa saa za New York, Guterres alitaka pande zote zijizuie kuendesha operesheni za kijeshi. Katibu Mkuu wa UN amesema dunia haiko tayari kushuhudia mzozo wa kijeshi kati ya India ya Pakistan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake kuhusu operesheni za kijeshi zinazofanywa na jeshi la India kwenye mstari wa usimamizi na mpaka wake wa kimataifa na Pakistan.

3492974

Kishikizo: kashmir india pakistan vita
captcha