IQNA

Warsha ya Mazingira kwa Mtazamo wa Qur'ani yafanyika Qatar

11:44 - February 19, 2020
Habari ID: 3472487
TEHRAN (IQNA) – Warsha ya 'Mazingira kwa Mtaamo wa Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad SAW imefanyika nchini Qatar.

Kwa mujibu wa taarifa, warsha hiyo imeandaliwa na Wizara ya Wakfu ya Qatar katika Msikiti wa Imam Muhammad bin Abdul Wahab, katika mji mkuu, Doha.

Wanazuoni kadhaa wa Qatar wameshiriki katika warsha hiyo wakiwemo Sheikh Nureddin al-Khademi na Sheikh Muhammad Rashedi ambao wamefafanua namna Uislamu unavyohimiza utunzwaji mazingira. Wanazuoni hao wametoa maelezo kuhusu aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad SAW zinavyozungumzia mazingira. Kati ya aya ambazo wanazuoni hao wamefafanua ni ile  sehemu ya aya ya 61 ya  Sura Hud isemayo: "… Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha,…"

Hii ilikuwa warsha ya siita ya aina hiyo ambayo imeandaliwa katika msikiti huo ili kuelimisha umma kuhusu masuala ya kidini yanayohusua maisha ya kila siku.

3879749

captcha