IQNA

Qur'ani Tukufu

Ukosefu wa msaada wa kifedha wasababisha kufungwa kwa TV ya Qur’ani Qatar

23:11 - July 23, 2022
Habari ID: 3475529
TEHRAN (IQNA) - Mkurugenzi kituo kimoja cha televisheni ya Qur’ani nchini Qatar ametangaza kukomeshwa kwa programu za kituo cha Runinga.

Youssef al-Shaibani alisema hatua hiyo ilichukuliwa kwa sababu msaada wa uliokuwa ukitolewa kuendesha televisheni hiyo umesitishwa.

Kituo cha televisheni, kinachoitwa Dohat al-Qur’an, kimekataa pendekezo la msaada kutoka taasisi moja ya Kikristo ya Marekani, alisema.

Shaibani alibaini kuwa baada ya uzinduzi wake mnamo 2020, Dohat al-Quran TV ilipokea msaada wa kifedha kutoka kwa mhisini ambaye alisitisha misaada yake baada ya mwaka.

Mfadhili mwingine alilipa gharama zote za utangazaji, ambazo ni pamoja na kodi ya satelaiti, kodi ya makao makuu ya kituo na mishahara ya wafanyikazi, kwa miezi sita, ameongeza.

Tangu wakati huo, wafanyikazi wa kituo hicho waliendelea na shughuli zao bila kulipwa, na kwa matumaini ya kupata thawabu na ujira kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa watumishi wa Qur’ani Tukufu.

Shaibani alisema kodi ya makao makuu ya kituo hicho haijalipwa katika kipindi hiki na hivyo hawana budi ila kufunga TV ya Dohat al-Qur’an.

Anaongeza kuwa gharama ya kodi ya satelaiti ndiyo sababu kuu ya kufungwa, kwani ni ni karibu  QR 50,000 kwa mwezi katika ya QR 150,000 zinazohitajika kuendesha kanali hiyo.

Amesikitika kuchukua uamuzi huo wakati kituo kilikuwa kimepata umaarufu, na kuvutia mamilioni ya watazamaji kutoka ulimwengu wote wa Kiarabu.

 

4072630

captcha