IQNA

Mazingira

Kituo cha Kiislamu nchini India chataka mazingira yahifadhiwa ili kuzuia joto kali

16:40 - June 04, 2024
Habari ID: 3478932
IQNA - Kituo cha Kiislamu nchini India kimewataka Waislamu kuhifadhi mazingira ili kupambana na wimbi la joto kali ambalo nchi hiyo inakabiliana nalo.

IQNA - Kituo cha Kiislamu nchini India kimewataka Waislamu kuhifadhi mazingira ili kupambana na wimbi la joto kali ambalo nchi hiyo inakabiliana nalo.

Katika kukabiliana na hali ya joto kali iliyoikumba maeneo ya kaskazini mwa India, hali ya joto ikiongezeka zaidi ya nyuzi joto 45°C (digrii 113 Selsiasi), moja ya vituo vikuu vya Kiislamu nchini humo kimetoa wito kwa Waislamu kujiepusha na kukata miti au kuchoma moto mashamba baada ya kuvuna.

Mpango huu unalenga kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto ambalo tayari limegharimu maisha ya watu wengi kutokana na joto kali.

Sheikh Khalid Rasheed Farangi Mahal, Mwenyekiti wa Kituo cha Kiislamu cha India, alisisitiza umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na kusema, "Kila Muislamu lazima ahakikishe hakuna miti ya kijani kibichi na mazao yanayochomwa moto."

Sheikh Mahal, msomi mashuhuri kutoka Lucknow, alitangaza fatwa hiyo Jumapili, akiangazia agizo la Qur'ani Tukufu kwa Waislamu kuhifadhi maeneo ya kijani kibichi na rasilimali za maji.

Fatwa hiyo ambayo ilitolewa kwa lugha ya Kiurdu na Kihindi inasema kwa uwazi, "Kuchoma moto miti na mimea ni haramu katika Uislamu na inachukuliwa kuwa dhambi kubwa."

Sheikh Mahal pia alitoa wito kwa viongozi wa dini ya Kiislamu kuzingatia utunzaji wa mazingira katika hotuba zao.

Ujumbe huu unakuja wakati mgumu huku mahakama ya India hivi majuzi ikiishinikiza serikali kutangaza hali ya dharura ya kitaifa kutokana na wimbi la joto linaloendelea.

Mahakama ilikosoa mamlaka kwa hatua zao duni za kuwalinda watu kutokana na hali ya joto kali.

Mahakama Kuu ya Rajasthan, jimbo ambalo limekumbwa na joto kali zaidi, ilionyesha wasiwasi wake juu ya kushindwa kwa serikali kujibu kwa ufanisi changamoto ya joto kali.

India, ambayo imezoea halijoto ya juu ya kiangazi, sasa inakabiliwa na mawimbi ya joto ambayo yanazidi kuwa ya muda mrefu, ya mara kwa mara, na makali kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa an tabianchi.

Watafiti wanaonya kwamba athari mbaya za mawimbi haya ya joto, yanayochochewa na shughuli za wanadamu za uchafuzi wa mazingira na kuharibu misitu.

3488613

Habari zinazohusiana
Kishikizo: mazingira uislamu
captcha