IQNA

Saudia inapanga kuwanyonga vijana waliokamatwa wakiwa watoto

8:37 - March 04, 2020
Habari ID: 3472529
TEHRAN (IQNA) – Saudi Arabia inakusudia kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya vijana watano ambao walikamatwa miaka kadhaa iliyopita wakiwa watoto wadogo.

Shirika lisilo la kiserikali la 'European Saudi Organisation for Human Rights (ESOHR)' lenye ofisi yake mjini London na Berlin limetoa onyo kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya vijana hao wenye umri mdogo, ambapo mwendesha mashtaka mkuu wa Saudi Arabia ametaka kutolewa adhabu kali dhidi yao. Kwa mujibu wa shirika hilo, kwa akali hadi sasa serikali ya Riyadh imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya watoto 10 wenye umri mdogo ambao iliwahukumu bila kufanyika vikao vya kiuadilifu vya mahkama. Shirika la ESOHR limefafanua kuwa vijana hao wako katika hali mbaya ikiwemo kushikiliwa kwa muda mrefu bila ya kufikishwa mahakamani sambamba na kunyimwa haki yao ya kuwa na mawakili wao wa utetezi, kuteswa, kufanyiwa miamala isiyo ya kibinaadamu na kushikiliwa katika seli za mtu mmoja.

Muhammad Issam Al-Faraj aliyezaliwa mwaka 2002 ni mmoja wa vijana hao waliohukumiwa kifo kwa kosa la kushiriki mazishi ya mmoja wa wahanga wa mauaji yaliyo kinyume cha sheria akiwa na umri wa miaka tisa. Mauaji hayo yalifanywa na kikosi maalumu cha Saudia mwaka 2012 katika mji wa Waislamu wa Kishia wa Al Qatif nchini humo. Muhammad Al-Faraj na Ali Aal Bati aliyezaliwa mwaka 1999 wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na watu wanaofuatiliwa na utawala wa kidikteta wa Aal Saud, huku Muhammad Aal Nimr aliyezaliwa mwaka 1998 naye akituhumiwa kushiriki mazishi ya mmoja wa wahanga wa mauaji ya kikatili yaliyofanywa na maafisa wa utawala wa Saudia.

3470823

Kishikizo: saudi arabia mashia iqna
captcha