IQNA

'Saa ya Qur'ani' kuwasaidia Waislamu kutafaakri kuhusu Qur'ani Tukufu

18:08 - May 13, 2020
Habari ID: 3472761
TEHRAN (IQNA) – Pamoja na kuwepo tishio la ugonjwa wa COVID-19 na matatizo yatokanayo na zuio la watu kutoka nje nchini Malaysia, Waislamu nchini humo wanatumia wakati wao nyumbani kujikurubisha zaidi na Qur’ani Tukufu.

Kati ya harakati ambazo Waislamu wameandaa mtandaoni ni World #QuranHour yaani  ‘Saa ya Qur’ani Duniani’. Harakati hiyo imeanzishwa na Warisan Ummah Ikhlas Foundation (WUIF)  ili kuwawezesha Waislamu kujifunza  Qur’ani Tukufu.

Leo,  mjumuiko huo wa intaneti utafanyika chini ya kauli mbiu ya ‘Kuanzisha Tena Maelewano Duniani’ ambapo washiriki kutoka Malaysia watasoma Sura Ar-Rahman na kuangazia maana ya kila aya.

Mkurugenzi wa WUIF Marhaini Yusoeff amesema mjumuiko huo wa saa nzima ambao hufanyika 20 Ramadhani ni kilele cha harakati ya mwaka mzima ya ‘Maingiliano na Qur’ani’ .

Wasimamizi wa harakati hiyo tukufu wanasema lengo lao kuu ni kuonyesha walimwengu kuwa sura zote 114 za Qur’ani Tukufu ni muongozo kamili kwa maisha ya mwanadamu. Aidha wanawahimiza Waislamu kusoma, kuelewa na kutekeleza mafundisho ya Qur’ani maishani.

3471413

captcha