IQNA

Kiongozi wa Hamas alaani vikwazo vya kidhulma vya Marekani dhidi ya Iran ataka viondolewe

12:25 - March 22, 2020
Habari ID: 3472591
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS usiku wa kuamkia leo amezungumza kwa simu na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu na kulaani vikali vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

Mbali na kulaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran, Ismail Hania amesisitiza kuwa, vikwazo hivyo ni vya kidhulma na inabidi vifutwe.

Vile vile amesema, taifa la Palestina liko pamoja na taifa la Iran katika juhudi zake za kupambana na kirusi cha corona.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amehimiza kukomeshwa kuzingirwa Ukanda wa Ghaza na vile vile ametaka kuachiliwa huru mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za kutisha za utawala wa Kizayuni wa Israel ambao hivi sasa usalama wao umezidi kuwa hatarini kutokana na maambukizi ya kirusi hatari cha corona.

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia jana Jumamosi ilitoa tamko rasmi na kuitaka Marekani ifute vikwazo vyake vya kidhulma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hasa wakati huu ambapo dunia nzima imo katika mapambano makali ya kuangamiza ugonjwa wa COVID-19.

Vikwazo haramu na vya kidhulma vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran vinajumuisha pia bidhaa muhimu hata dawa na vifaa vya tiba, suala ambalo limewasababishia matatizo mengi wananchi wa Iran hasa wagonjwa wa COVID-19.

Licha ya Iran kupiga hatua kubwa za kisayansi na kiteknolojia na kuwa na madaktari bingwa wa kila namna, lakini vita dhidi ya kirusi cha corona vinahitaji ushirikiano wa kimataifa. Cha kuudhi ni kuwa, viongozi wa Marekani hawana utu na hawajali suala hilo.

3886826

captcha