IQNA

‘Quranona’, Aplikesheni Mpya ya Qur’ani yazinduliwa

11:56 - April 19, 2020
Habari ID: 3472680
TEHRAN (IQNA) – Aplikesheni mpya ya Qur’ani Tukufu inayojulikana kama “Quranona” ambayo ina tarjuma kwa lugha 35 imezinduliwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, aplikesheni hiyo ya simu za mkononi ina sauti za wasomaji au maqarii 250. Halikadhalika aplikesheni hiyo ambayo inaweza kutumiwa katika simu zenye mfumo wa android au iOS pia ina tafsiri 8 za Qur’ani Tukufu na sehemu maalumu ‘Mwalimu wa Qur’ani’ kwa ajili ya watoto.   

Aplikesheni hiyo inawapa watumizi fursa ya kuchagua rangi za kurasa za Qur’ani wakati wa kusoma na pia kuna uwezekano wa kukopi na kuwatumia wengine aya za Qur’ani.  Sifa nyingine aya aplikesheni hiyo ni hadithi 24 za Qur’ani kwa watoto sambamba na program ya kupaka rangi na na kujibu maswali kutoka hadithi zilizopo. Aidha aplikesehni hiyo inatoa mafunzo ya kuhifadhi aya za Qur’ani Tukufu inamuwezesha mtumizi kusoma Qur’ani Tukufu kwa Kiarabu na iwapo atakosea atasahihishwa. Pia aplikesheni hiyo ina Dua 50 za Qur’ani Tukufu na Sunna.

Unaweza kuipata aplikesheni hiyo kupitia njia ziifuatazo:

Android:https://t.co/OJA2xXaOsz

IOS:https://t.co/OohFG8dSQu

3891964/

captcha