IQNA

14:26 - June 15, 2020
Habari ID: 3472865

Maandamano Uholanzi kuunga mkono Palestina

TEHRAN (IQNA) –Mamia ya watu wameshiriki katika maandamano mjini Amsterdam Uholanzi Jumapili na kutangaza kuunga mkono Wapalestina huku wakipinga mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel kupora ardhi zaidi za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Maandamano Uholanzi kuunga mkono Palestina

Waandamanaji wameulaani vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Aidha wametaka hatua za kivitendo zichukuliwe kusitisha sera kandamizi na za kibaguzi za Israel na pia kusitishwa uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo wa Kizayuni.

Halikadhalika washiriki wamelaani kila aina ya ubaguzi duniani hasa mfumo wa ubaguzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Palestina.

Maandamano Uholanzi kuunga mkono Palestina

3904999

captcha