IQNA

Wanajeshi wa Israel wamuua shahidi Mpalestina katika ukingo wa Magharibi

17:36 - July 10, 2020
Habari ID: 3472947
TEHRAN (IQNA) - Mpalestina ameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Kwa mujibu wa taarifa,   Ibrahim Moustapha Abou Yacoub, 29,  ameuawa kwa kupigwa risasi shingono na wanajeshi wa Israel katika kijiji cha Kifl Hares, kusini mwa Nablus.

Wakati huo huo, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, kuuawa shahidi Wapalestina ni ishara ya wazi ya kushikamana kwao na mapambano na muqawama dhidi ya utawala ghasibu wa Israel. Hazim Qassim amesema hayo akizungumzia kuuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel kijana wa Kipalestina kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, kuuawa shahidi Wapalestina kunaweka wazi ukweli huu kwamba, wananchi wa Palestina katu hawakubali kusalimu amri mbele ya siasa za ukandamizaji na utwishaji mambo zautawala wa Kizayuni wa israel.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Chama cha Hamas ameeleza kwamba, kujitolea wananchi Wapalestina ni nguvu ya wazi kabisa ya kuzishinda njama mtawalia za utawala dhalimu wa Israel unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu kibla cha kwanza cha Waislamu.

Kwa mujibu wa Jumuiya ya Taifa ya Familia za Kipalestina, Wapalestina 149 waliuawa shahidi na askari wa utawala haramu wa Israel mwaka uliopita wa 2019, ambapo asilimia 74 miongoni mwao walikuwa wanatoka Ukanda wa Ghaza.

Aidha taasisi hiyo ya kutetea haki za Wapalestina imesema kuwa, asilimia 23 ya Wapalestina waliouawa shahidi mwaka jana ni watoto wadogo.

Sera za utawala ghasibu wa Israel za kuwashambulia na kuwaua shahidi kwa kuwapiga risasi Wapalestina zinakwenda sambamba na mipango yake ya kupora na kughusubu ardhi zaidi za Wapalestina sanjari na kupanua ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni.

3471946

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha