IQNA

Rais wa Palestina alaani mapatano ya UAE-Israel, ayataja kuwa ya kipuuzi

21:55 - August 19, 2020
Habari ID: 3473083
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas amelaani mapatano ya hivi karibuni yaliyofikiwa ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na utawala haramu wa Israel na kuyataka kuwa ya kipuuzi na yasiyo na maana kwa Wapalestina.

Akizungumza Jumanne katika mji wa Ramallah katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu amesema: “Hatujalishwi na upuuzi unaoendelea huku na kule, hasa siku za hivi karibuni wakati mapatano ya pande tatu yalipotangazwa kati ya UAE, Isreal na Marekani kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Israel na UAE.”

Kati kauli yake mbele ya umma baada ya mapatano hayo kutangazwa wiki iliyopita, Abbas aliituhumu UAE kuwa imewasaliti Wapalestina ambao kwa muda mrefu ardhi zao zinakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.”

“UAE imewasaliti Wapalestina kuhusu mambo yote ikiwa ni pamoja na Quds (Jerusalem) Tukufu.”

Itakumbukwa kuwa, Alhamisi iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kufikiwa mapatano baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala haramu wa Israel kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia baina ya pande mbili, hatua ambayo imeendelea kulaaniwa na kulalamikiwa katika kila kona ya dunia.

3472324

Kishikizo: abbas palestina uae
captcha