IQNA

22:26 - August 16, 2020
Habari ID: 3473075
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wenye hasira nchini Libya wameteketeza moto jengo la ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) mjini Tripoli wakilalamikia hatua ya serikali ya Abu Dhabi ya kufikia makubaliano ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala dhalimu wa Israel.

Taarifa zaidi kutoka nchini Libya zinasema kuwa, wananchi wenye hasira jana waliuvamia ubalozi wa Imarati mjini Tripoli na kuchoma moto sehemu ya jengo la ubalozi huo wakionyesha upinzani wao dhidi ya nchi hiyo wa kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel unaotenda jinai kila leo dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina.

Picha zilizoenezwa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio hilo zinaonyesha jinsi jengo la ubalozi wa Imarati mjini Tripoli Libya lilivyoharibiwa vibaya.

Wakati huo huo malalamiko ya walimwengu yameendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya dunia dhidi ya hatua ya nchi ya Imarati ya kufikia makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Huko Afrika Mashariki pia, Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina imelaani vikali mapatano yaliyofikiwa baina ya watawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala ghasibu wa Israel chini ya usimamizi wa makundi ya Kizayuni nchini Marekani.

Halikadhalika, mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini amekosoa mapatano ya kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Imarati na utawala haramu wa Israel.

Mandla Mandela amekosoa vikali mapatano hayo na kusema ni fikra ya kijinga kuamini kwamba mapatano ya Imarati na Israel ya kuanzisha uhusiano yanaimarisha amani katika eneo la magharibi mwa Asia.

Mandla Mandela amesisitiza kuwa amani haiwezi kupatikana katika eneo hilo la Asia bila ya kutambuliwa kikamilifu haki za kimsingi za watu wa Palestina.  

Itakumbukwa kuwa, Alhamisi iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kufikiwa mapatano baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu na utawala haramu wa Israel kuhusu kuanzishwa uhusiano wa kawaida wa kidiplomasia baina ya pande mbili, hatua ambayo imeendelea kulaaniwa na kulalamikiwa katika kila kona ya dunia.

3916805

 

سفارت امارات در طرابلس به آتش کشیده شد + عکس

سفارت امارات در طرابلس به آتش کشیده شد + عکس

سفارت امارات در طرابلس به آتش کشیده شد + عکس

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: