IQNA

Baba na mtoto wasoma aya ya Surah Fath kumhusu Mtume Muhammad SAW

12:29 - November 05, 2020
Habari ID: 3473332
TEHRAN (IQNA) – Kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW maarufu kama Milad-un-Nabii na wiki ya Umoja wa Waislamu, qarii maarufu wa Iran Mehdi Gholamnejad amesema aya ya 29 ya Surah al Fath akiwa na mtoto wake.

Katika klipu ambayo imerushwa katika mitandao ya kijamii wawili hao wamesikika wakisema sehemu ya aya ya 29 ya Surah Al Fath katika Qur'ani Tukufu inayosema hivi: "Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao…"

Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kuwa Mtume Muhammad SAW alizaliwa 12 Rabiul Awwal nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa ni 17 Rabiul Awwal.

Kwa msingi huo, Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya Umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa Waislamu kote duniani.

3932852

captcha