IQNA

Maulid ya Mtume Muhammad (SAW)

Kongamano la 'Maisha ya Mtume Muhammad (SAW)' Kufanyika Birmingham Septemba Mosi

20:53 - August 28, 2023
Habari ID: 3477510
BIRMINGHAM (IQNA) - Kundi la wanazuoni, wasomi, na viongozi wa kidini na wa kijamii kutoka duniani kote wanakutana mwezi ujao katika Kongamano la kwanza la kila mwaka la "Maisha ya Mtume Muhammad (SAW)", tukio lililopangwa kubadilishana maarifa na kubadilishana maoni kati ya Waislamu na wasio Waislamu.

Kongamano hilo limepanta na Kituo cha Televisheni cha  Islam Channel limepangwa kufanyika Jumamosi, Septemba 30, katika  ukumbi wa ICC Birmingham.

"Kongamano hilo litafanyika sambamba na  maadhimisho ya Maulid au Mazazi ya Mtume Muhammad (SAW) katika mwezi wa Rabi' Al-Awwal na litaangazia maisha yake, urithi na mafundisho yake.”

"Hii itakuwa fursa ya kipekee kwa Waislamu na wasio Waislamu kujumuika pamoja na kubadilishana mawazo."

Wazungumzaji ni pamoja na Mohamed Ali Harrath, mwanzilishi wa Islam Channel, Jonam Van Klaveren, Naima Roberts, Prof. Joel Hayward, Dk. Musharraf Hussain OBE, na wengine.

Waislamu wengi wanaona siku ya kuzaliwa Mtume kama fursa ya kujifunza na kutafakari juu ya maisha ya Muhammad Muhammad (SAW).

3484944

Habari zinazohusiana
captcha