IQNA

16:58 - November 07, 2020
News ID: 3473337
TEHRAN (IQNA) - Mahmoud Shahat Anwar, qarii maarufu wa Misri amehudhuria sherehe za kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW maarufu kama Maulidi ambapo na kusoma aya za Qur'ani.

Katika sherehe hizo zilizofanyika Alhamisi Novemba 5 2020 katika jimbo la Sharqia kaskazini mwa Misri, alisoma aya za Surah al Kahf na Taha.

Sheikh Mahmoud Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Afrika Kusini, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

3928964

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: