IQNA

Afisa mwandamizi wa Palestina, Saeb Erekat Dies afariki kwa corona

16:27 - November 10, 2020
Habari ID: 3473347
TEHRAN (IQNA) – Afisa mwandamizi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Saeb Erekat ameaga dunia leo baad ya kuumbukizwa corona.

Erekat ambaye alipata umashuhuri kama mwakilishi wa  Palestina katika  mazungumzo ya kimataifa ameaga dunia hospitalini akiwa na umri wa miaka 65. Kifo chake kimetangazwa kupitia taarifa ya Chama chake cha Fatah.

Erekat alishiriki katika takriban juhudi zote za kusaka amani kati ya utawala haramu wa Israel na Wapalestina, kuanzia mkutano wa kihistoria uliofanyika Madrid mwaka 1991, ambapo alihudhuria akiwa amejifunika kitambaa cha kufunga kichwani chenye miraba ya rangi nyeusi na nyeupe ambayo ni ishara ya utaifa wa Wapalestina.

3934380

captcha