“Taifa la Iran lenye hamasa na uaminifu, kama mlivyoarifiwa, hati ya makubaliano imetiwa saini kati ya marais wa Iran na Marekani,” Ayatullah Khamenei alisema katika ujumbe uliotolewa siku ya Alhamisi.
“Katika kufikia hatua hii, maafisa wetu walifanya juhudi nyingi kwa huruma na nia njema, na bila shaka rais wa Marekani ndiye aliyekuwa akitumia nyenzo na shinikizo mbalimbali kwa sababu ya kukata tamaa ili kufanikisha jambo hilo.”
Hati hiyo ya makubaliano ilitiwa saini kwa njia ya mawasiliano ya mbali au kidijitali kati ya Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na Rais wa Marekani Donald Trump. Makubaliano hayo yanataka kukomesha kabisa uhasama katika nyanja zote ikiwemo Lebonon, kuondolewa kwa mzingiro wa majini wa Marekani ndani ya siku 30, kurejeshwa kwa usafiri wa kibiashara kupitia Mlango wa Bahari wa Hormuz, mpango wa ujenzi upya wenye thamani ya angalau dola bilioni 300, pamoja na kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani.
Ayatullah Khamenei amesema alikuwa na mtazamo tofauti kuhusu suala hilo, lakini aliridhia makubaliano hayo kutokana na ahadi zilizotolewa na Rais Pezeshkian, ambaye kama mkuu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa aliahidi kwa niaba yake na wanachama wengine kulinda haki za taifa la Iran na kambi ya muqawama.
Rais Pezeshkian pia amesisitiza kuwa hatakubali madai yoyote ya ziada kutoka upande wa Marekani, Kiongozi huyo alisema.
“Kuanzia sasa, sisi, yaani ninyi taifa lenye heshima na mimi mtumishi wenu mnyenyekevu, tutasubiri utekelezaji wa masharti yaliyotajwa. Hata hivyo ni wazi kwamba mazungumzo ya ana kwa ana yatakayofanyika siku zijazo hayatamaanisha kukubali mtazamo wa adui,” Ayatullah Khamenei alisema.
“Tuna matumaini kuwa kwa baraka za dua za Bwana wetu, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake kutukufu), ushindi na mafanikio mbalimbali yataipata taifa tukufu la Iran.”
Kwa mujibu wa hati hiyo ya makubaliano, pande hizo mbili zimeanza kipindi cha siku 60 cha mazungumzo kwa lengo la kufikia makubaliano ya mwisho na ya kina. Mazungumzo ya ana kwa ana yanatarajiwa kuanza tarehe 19 Juni nchini Uswisi, huku Pakistan na Qatar zikitarajiwa kuwa wapatanishi.
Makubaliano hayo yalifikiwa kufuatia vita vya ugaidi vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Israel dhidi ya Iran mwishoni mwa mwezi Februari.
3497890