IQNA

Familia mbili za Wayemen zaishtaki Marekani kwa kuwaua jamaa zao 34 wakiwemo watoto

17:43 - January 29, 2021
Habari ID: 3473601
TEHRAN (IQNA)- Familia mbili za Wayemen zimewasilisha mashtaka dhidi ya Marekani baada ya jamaa zao 34, wakiwemo watoto 17 kuuawa katika hujuma za ndege za kivita za Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa familia hizo zinasema ziliwapoteza jamaa zao hao baina ya mwaka 2013 na 2018 katika oparesheni za ndege za kivita zisizo na rubani za Marekani. Mashtaka hayo yamewasilishwa na  shirika la kutetea haki za binadamu la Repreive kwa niaba ya familia hizo. Mashtaka hayo yamewasilishwa katika Tume ya Haki za Binadamu Bara Amerika ambayo iko chini ya Jumuiya ya Mataifa ya Bara Amerika.

Katika shtaka hilo familia za Al-Ameri na Al-Taisy zimesema jumla ya watu 48 waliuawa katika hujuma hizo za Marekani ambapo miongoni mwa walipoteza maisha 34 ni jamaa zao wakiwemo watoto 34.

Familia hizo zinataka Marekani ishinikizwe isitishe mashambulizi zaidi nchini Yemen kwani watu wasio na hatia wanapoteza maisha.

Wakili wa shirika la Repreive Jennifer Gibson amesema mashambulizi hayo yalitekelezwa wakati wa utawala wa Barack Obama na pia wakati wa Donald Trump.  Katika moja ya mashambulizi Disemba 2013 wakati wa utawala wa Obama, ndege za kivita za Marekani zilishambulia msafara wa harusi na kuua watu 12, wakiwemo saba kutoka familia ya al-Ameri na watano kutoka familia ya al-Taisy.

Familia hizo zinataraji kuwa tume hiyo itachukua hatua ya awali ya kutambua kuwa jinai ilitendeka.

3473832

Kishikizo: yemen marekani
captcha