IQNA

19:40 - March 08, 2021
News ID: 3473715
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya kitengo cha wanawake katika Mashindano ya 37 Kimataifa ya Qur’ani ya Iran ilianza Jumapili.

Katika siku ya kwanza ya finali hizo kulikuwa na washiriki 13 kutoka  Indonesia, Mauritania, Nigeria, Ivory Coast, Chad, Burundi, Iran, Uganda, Pakistan, Senegal, Gambia, na Afghanistan.

Majaji katika kitengo cha wanawake ni kutoka  Iran, Jordan, Iraq, Syria, Indonesia na Malaysia.

Mashindano ya 37 Kimataifa ya Qur’ani  ya Iran yalianza Jumamosi 6 Machi na yanatazamiwa kumalizika Alhamisi 11 Macho.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ni 'Kitabu Kimoja, Ummah Mmoja".

Mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kwani kutokana na janga la  COVID-19 au corona, yanafanyika kwa njia ya Intaneti.

Zaidi watazamaji milioni 2.5 walifuatilia duru za mchujo za mashindano hayo kwa njia ya intaneti na inatazamiwa kuwa baina ya watu milioni 6-8 watafuatilia fainali ya mashindano hayo kwa njia ya intaneti.

3958125

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: