
Kamati ya Istihlal (uangalizi wa mwezi) iliyo chini ya Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ilitangaza Jumatano jioni kuwa hilali ya Ramadhani imeonekana, na hivyo Alhamisi, tarehe 19 Februari, ikathibitishwa kuwa mwanzo wa mwezi mtukufu.
Vilevile, ofisi ya Marjaa wa juu wa Kishia nchini Iraq, Ayatollah Ali al‑Sistani, ilitangaza Alhamisi kuwa siku ya kwanza ya Ramadhani.
Hata hivyo, nchi kadhaa za Kiislamu, zikiwemo Saudi Arabia, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Syria, Lebanon na Palestina, zilianza kufunga Jumatano, kufuatia mitazamo yao katika kuthibitisha mwanzo wa mwezi. Wanazuoni wa Kiislamu wana mitazamo tofauti kuhusu kuanza kwa miezi ya kalenda ya Hijria; baadhi yao hutegemea hesabu za kielimu za astronomia, huku wengi wakisisitiza kuonekana kwa macho kwa mwezi mwandamo kama msingi wa kisheria.
Ramadhani ni mwezi wa tisa na mtukufu zaidi katika kalenda ya Kiislamu, ambapo Waislamu huadhimisha kuteremshwa kwa Qur’ani Tukufu kwa Mtume Muhammad (SAW).
Habari inayohusiana:
Katika mwezi huu mtukufu, Waislamu hufunga kuanzia alfajiri hadi machweo ya jua, wakijiepusha na kula, kunywa na kuvuta sigara. Aidha, huongeza juhudi katika swala, dua, sadaka na matendo mema, wakilenga kuimarisha imani yao na kusafisha nyoyo na roho zao.
3496469