IQNA

Ramadhani Kuanza Februari 19 Nchini Saudi Arabia kwa Mujibu wa Hesabu za Kiastronomia

11:31 - February 10, 2026
Habari ID: 3481914
IQNA – Wakati mamilioni ya Waislamu duniani kote wakisubiri kwa hamu kuwasili kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na maandalizi yakiendelea, hesabu za kiastronomia zinaonesha kuwa mwisho wa mwezi wa Shaaban 1447 Hijria kiastronomia utasadifiana na Jumatano, Februari 18.

Kwa mujibu wa makadirio hayo, siku ya kwanza ya mwezi wa saumu itakuwa Alhamisi, Februari 19.

Kwa mujibu wa Dalil Al-Saudiyya, na kwa kuzingatia hesabu za kiastronomia, Ramadhani ya mwaka huu itakuwa na siku 30 kamili, huku Jumamosi, Machi 21, 2026 ikitarajiwa kuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal, unaoadhimishwa kwa Sikukuu ya Eid al-Fitr.

Profesa Mohammed Gharib, mtaalamu wa utafiti wa kiastronomia katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Astronomia na Jiografia ya Saudi Arabia, alieleza kuwa hesabu za kiastronomia zinaonesha kuwa mwezi wa Shaaban huenda ukawa na siku 30, akiongeza kuwa kiastronomia, siku ya kwanza ya Ramadhani inatarajiwa kusadifiana na Februari 19.

Habari inayohusiana:

Hata hivyo, mtaalamu wa hali ya hewa Khalid Al-Zaaq amesema kuwa data zinaonesha kuwa Jumatano, Februari 18 huenda ikawa mwanzo wa Ramadhani, na iwapo mwezi wa siku 30 utakamilika, basi Ijumaa, Machi 20, 2026 itakuwa siku ya Eid al-Fitr.

4333295

captcha