IQNA

Mtanzania ashinda mashindano ya Qur’ani Qatar, apata zawadi kubwa

19:30 - May 10, 2021
Habari ID: 3473896
TEHRAN (IQNA)- Qarii Mtanzania ameibuka mshindi katika duru ya nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Taasisi ya Kijiji cha Utamaduni (Katara) nchini Qatar.

Kwa mujibu wa taarifa washindi watano wametangazwa miongoni mwa kundi kubwa la walioshiriki katika mashindano hayo ya kila mwaka ambayo yamefanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa taarifa, nafasi ya kwanza imechukuliwa na Abdullah Dawod Mohammed wa Tanzania. Amefuatiwa na Alaa Adin Hamza Magazi Hamtour wa Misri huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Hamza Warrash wa Morocco. Nafasi za nne na tanzo zimeshukwa na Mohammad Hashim Mohammad Bulair wa Uturuki na Omer Aksukos wa Morocco kwa taratibu.  Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki  jumla 2,004 ambapo 18 walikuwa kutoka nchi za Kiarabu na 44 kutoka nchi zisizo za Kiarabu. Washiriki 25 waliofika nusu fainali walikuwa ni kutoka Morocco, Iran, Iraq, Misri, Syria, Ufilipino, Indonesia, Algeria, Jordan, Pakistan, Tanzania, Libya, Uturuki, na Yemen.

Aliyeshika nafasi ya kwanza amepata Riali za Qatar (QR) nusu milioni huku alisyeshika nafasi ya pili akipata QR 400,000 na aliyeshika nafasi ya tatu amepata QR 300,000. Walioshika nafasi za nne na tano wamepata QR, 200,000 na QR 100,000 kwa taratibu.

Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Katara ni mashuhuri katika ulimwengu wa wa Kiislamu ambapo washindi hutangazwa katika televisheni ya Qatar.

Mbali na mashindano ya Qur'ani Taasisi ya Katara pia huandaa mashindano ya mashairi ya Kiarabu na pia taasisi hiyo imetayarisha kipindi maarufu cha katuni ambacho kinajulikana kama Tamour na Tamoura.

Mashindano ya Qiraa ya Qur’ani ya Taasisi ya Katara yalianzishwa kwa lengo la kuwashajiisha usomaji Qur’ani Tukufu na pia kutambua vipaji vilivyopo.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Qatar ni mfadhili mkuu wa mashindano hayo ambayo mwaka huu pia yamefanyika katika fremu ya shughuli za “Doha, Mji Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu.”

3474673

Kishikizo: qatar ، katara ، mashindano ya qurani
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :