IQNA

Waislamu Kenya wakusanya misaada kwa ajili ya Wapalestina Ghaza

18:10 - June 07, 2021
Habari ID: 3473986
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Kenya wametangaza kuunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina hasa baada ya hujuma ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel

 Katika kutekeleza kivitendo uungaji mkono huo, asasi hizo za Kiislamu zimekusanya misaada ya kifedha kutoka kwa Waislamu nchini humo kwa ajili ya kuwasaidia Wapalestina wa Ghaza ambao hivi karibuni walikabliwa na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taasisi hizo za Kiislamu kwa kushirikiana pamoja kwa kushirkiana na maimamu na pia benki za Kiislamu nchini humo zimekusanya nguo, vyakula, vifaa vya tiba na fedha taslimu Ksh milioni mbili kwa ajili ya kuunga mkono familia za Wapalestina wanaoteseka Ghaza.

Wakati wa vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza vilivyoanza Mei 10 mwaka huu na kuendelea kwa siku 12, wananchi wa Kenya, hasa Waislamu waliandamana katika miji ya Nairobi kulaani vikali jinai hizo za Israel dhidi ya Wapalestina.

3976041/

Kishikizo: kenya ، palestina ، ghaza
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha