IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Sherehe ya Kuwaenzi Washindi wa Mashindano ya Qur’ani nchini Kenya

23:05 - August 24, 2024
Habari ID: 3479322
IQNA - Sherehe ilifanyika katika mji mkuu wa Kenya wa Nairobi kuwaenzi washindi wa mashindano ya hivi karibuni ya Qur'ani.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni (MWL) Sheikh  Muhammad bin Abdul Karim Issa alikuwepo kwenye sherehe hiyo.

Mashindano hayo yalikuwa yamefanyika mapema mwaka huu chini ya kauli mbiu ya ‘wasomi wa mitindo kumi ya usomaji wa Qur’ani’ kwa kushirikisha idadi kubwa ya wahifadhi wa Qur’ani kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Mashindano hayo yalilenga kuwatia moyo wahifadhi Qur'ani ambao wana ustadi wa mitindo kumi ya usomaji wa Qur'ani.

Kukuza mafundisho ya Qur’ani Tukufu na kuinua vizazi vyenye uwezo wa Qur'ani yalikuwa miongoni mwa malengo mengine ya mashindano hayo.

Katika hotuba yake katika hafla hiyo, mkuu wa MWL alisisitiza kutafakari na kuhusu Qur'an na kufanyia kazi mafundisho yake.

Kenya ni nchi ya Afrika Mashariki yenye ukanda wa pwani kwenye Bahari ya Hindi. Uislamu ni dini ya zaidi ya asilimia 11 ya wakazi wa Kenya, au takriban watu milioni 4.3.

3489625

Habari zinazohusiana
Kishikizo: kenya qurani tukufu
captcha